Ephesians 2:1-3

Tumefanywa Kuwa Hai Ndani Ya Kristo

1 aKwa habari zenu, mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu, 2 bambazo mlizitenda mlipofuatisha namna ya ulimwengu huu na za yule mtawala wa ufalme wa anga, yule roho atendaye kazi sasa ndani ya wale wasiotii. 3 cSisi sote pia tuliishi katikati yao hapo zamani, tukitimiza tamaa za asili yetu ya dhambi na kufuata tamaa zake na mawazo yake. Nasi kwa asili tulikuwa wana wa ghadhabu, kama mtu mwingine yeyote.
Copyright information for SwhNEN